Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili March 29 2026

Joel JJ By Joel JJ • 29th March 2026


Tetesi za usajili Ulaya, Jumapili March 29 2026

Dirisha la usajili linazidi kupamba moto huku vilabu vikubwa vya Ulaya vikianza kupanga mikakati ya kuimarisha vikosi vyao. Hizi hapa ni tetesi kuu za leo kutoka vyombo mbalimbali vya habari:


Newcastle wamuwinda James Trafford

Newcastle United wanaendelea kuonyesha nia ya kumsajili mlinda lango wa England James Trafford (23), iwapo ataamua kuondoka Manchester City.
Chanzo: Football Insider


Sean Dycheakanusha kujiunga Tottenham

Kocha Sean Dyche amekanusha taarifa zinazomuhusisha na kuchukua nafasi ya Igor Tudor katika Tottenham Hotspur.
Chanzo: Talksport


Evan Ndicka awindwa na vigogo Ulaya

Beki wa AS Roma, Evan Ndicka (26), yuko kwenye rada za Barcelona, Tottenham Hotspur, Liverpool na Manchester United. Roma wako tayari kuuza kwa dau linalozidi pauni milioni 39.
Chanzo: CaughtOffside


Nyakossi avutia vilabu vya England

Beki wa Uswisi Roggerio Nyakossi (22), anayekipiga OH Leuven, anawindwa na Liverpool na Chelsea huku mkataba wake ukielekea ukingoni.
Chanzo: The Sun


Marcos Llorente ataka kubaki Atletico

Kiungo Marcos Llorente (31) anatarajiwa kuendelea kubaki Atlético Madrid, akiwa kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya licha ya kuvutiwa na vilabu vya Premier League.
Chanzo: Fichajes


Real Madrid wamfuatilia Adam Wharton

Real Madrid ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton (22), ambaye thamani yake inaendelea kupanda kwa kasi.
Chanzo: AS


Schlotterbeck karibu kuongeza mkataba Dortmund

Beki wa Ujerumani Nico Schlotterbeck (26), ambaye alikuwa akiwindwa na Liverpool na Real Madrid, anakaribia kusaini mkataba mpya na Borussia Dortmund utakaomuweka klabuni hadi mwaka 2031.
Chanzo: Florian Plettenberg


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.