Kiungo wa Real Madrid, Dani Ceballos, amefikia uamuzi wa kuondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, huku akionesha dhamira ya kurejea katika klabu yake ya zamani ya Real Betis.
Taarifa zinaeleza kuwa Ceballos anatamani kupata muda zaidi wa kucheza, jambo linalochangia uamuzi wake wa kutaka kuondoka Santiago Bernabéu na kurejea Betis ambako aliwahi kung’ara hapo awali.
Hata hivyo, uongozi wa Real Madrid hauko tayari kumruhusu mchezaji huyo kuondoka bure bila malipo, hivyo klabu yoyote itakayohitaji huduma yake italazimika kuwasilisha ofa rasmi ili kufanikisha usajili huo.
Ceballos bado ana mkataba unaoendelea hadi mwaka 2027, baada ya kuongeza kandarasi yake mwaka 2023, hali inayowapa Real Madrid nguvu katika mazungumzo ya uhamisho wake.
(Taarifa: @MARCA)



