Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa March 27 2026

Joel JJ By Joel JJ • 27th March 2026


Tetesi za usajili Ulaya, Ijumaa March 27 2026

Dirisha la usajili wa majira ya kiangazi linazidi kunoga barani Ulaya huku klabu kubwa zikianza kupanga mikakati yao mapema. Hizi hapa ni tetesi moto zilizotikisa soka la Ulaya leo Ijumaa, Machi 27, 2026:


Bayern Munich Wamkingia Kifua Michael Olise

Bayern Munich wamepuuza taarifa zinazoihusisha kuondoka kwa mshambuliaji wao Michael Olise kwenda Liverpool FC.
Inadaiwa hata dau la zaidi ya pauni milioni 170 halitatosha kumng’oa nyota huyo.
Chanzo: Talksport


Manchester United Wamvizia Sandro Tonali

Manchester United wanatarajia kuwasilisha ofa rasmi kwa Newcastle United kwa ajili ya kiungo Sandro Tonali mwishoni mwa msimu.
Chanzo: Daily Mail


Myles Lewis-Skelly Aingia Kwenye Radar ya United

United pia wanamfuatilia beki wa kushoto wa Arsenal FC, Myles Lewis-Skelly, ambaye hajapata nafasi ya kutosha kikosini.
Chanzo: Daily Express


Hatma ya Marcus Rashford Yazua Vita

Paris Saint-Germain na AC Milan wanafuatilia hali ya Marcus Rashford, huku wakisubiri kuona kama FC Barcelona watashindwa kumsajili moja kwa moja.
Wakati huohuo, Aston Villa nao wako tayari kumchukua iwapo watamkosa Jadon Sancho.
Chanzo: CaughtOffside / SportsBoom


Arsenal Wamtaka Julian Alvarez

Arsenal FC wana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julian Alvarez.
Chanzo: Football.London


Liverpool Wamvizia Iliman Ndiaye

Liverpool FC wanatajwa kumtaka mshambuliaji wa Everton FC, Iliman Ndiaye.
Chanzo: Teamtalk


Dili la Pauni Milioni 100 kwa United

Mbali na Ndiaye, Manchester United pia wanamfuatilia James Garner katika mpango wa usajili unaoweza kufikia pauni milioni 100.
Chanzo: Fichajes


Newcastle Wamtaka Ben White

Newcastle United wanamwona Ben White kama mbadala wa Kieran Trippier iwapo ataondoka.
Chanzo: SportsBoom


Arsenal Wawania Wachezaji Wawili

Arsenal wanamfuatilia pia Anthony Gordon wa Newcastle, huku wakitajwa kutokuwa na nafasi kubwa kwa Khvicha Kvaratskhelia wa PSG kwa sasa.
Chanzo: Sky Sports


Atletico Madrid Wamtaka Ferran Torres

Atletico Madrid wanapanga kumsajili Ferran Torres kutoka Barcelona.
Chanzo: Fichajes


Balde Awindwa na Vigogo

Beki wa FC Barcelona, Alejandro Balde, anawaniwa na Manchester United, Manchester City na Aston Villa.
Chanzo: Mundo Deportivo


Geertruida Aibua Vita ya Vilabu

Mchezaji wa RB Leipzig anayekipiga kwa mkopo Sunderland AFC, Lutsharel Geertruida, anawindwa na klabu kadhaa ikiwemo Liverpool, Aston Villa na Tottenham.
Chanzo: Teamtalk


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.