Yanga na Azam FC kukutana nusu fainali Muungano Cup

Joel JJ By Joel JJ β€’ 23rd April 2026


Yanga na Azam FC kukutana nusu fainali Muungano Cup

Mashabiki wa soka wanatarajia burudani ya hali ya juu baada ya Yanga SC na Azam FC kufuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Muungano. Mchezo huo mkubwa utapigwa Jumamosi, April 25 katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

Azam FC ilitinga nusu fainali Jumatano usiku baada ya kuichapa KVZ mabao 2-0 katika mchezo wa pili wa robo fainali, ikionyesha uimara mkubwa hasa katika safu ya ushambuliaji na nidhamu ya kujilinda.

Kwa upande wa Yanga, wao walikuwa wa kwanza kukata tiketi ya nusu fainali baada ya kuifunga Muembe Makumbi mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa Jumanne. Yanga walionyesha kiwango cha juu, wakitawala mchezo kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Sasa macho yote yanaelekezwa Zanzibar, ambapo dabi ya Dar es Salaam itahamia visiwani. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia ya timu hizi mbili pamoja na ubora wa vikosi vyao.

Je, Yanga wataendelea na makali yao au Azam FC watabadili upepo na kukata tiketi ya fainali ya michuano hiyo iliyoingia msimu wa tatu tangu iliporejeshwa rasmi?


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.