Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopita wa ligi kuu ya NBC, vinara wa ligi Yanga wanakabiliwa na mechi nyingine ngumu ugenini jijini Mwanza.
Ni mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa Jumatano April 08 katika uwanja wa CCM Kirumba.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kikosi cha timu kitaondoka jijini Dar es salaam kusiku wa leo Jumatatu kuelekea Mwanza tayari kwa mchezo huo.
Kamwe amesema wanatambua mchezo dhidi ya Pamba Jiji utakuwa mgumu lakini lengo lao ni kuvuna alama tatu ili kuendelea kujiimarisha juu ya msimamo wa ligi.
"Kikosi chetu kinaondoka jijini Dar es salaam leo saa 3 usiku kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo dhidi ya Pamba Jiji utakaopigwa CCM Kirumba April 09"
"Tumepata tena faida ya kuwa kileleni kwa tofauti ya alama tatu hvyo hatupaswi kurudia tena makosa"
"Tunafahamu ubingwa wa msimu huu unahitaji roho ngumu na mapambano makali ndani na nje ya uwanja. Nawaasa mashabiki watoke majumbani, tuwe mstari wa mbele kuisapoti timu yetu kila mechi." alisema Kamwe



