Msimu huu wa mashindano mbalimbali umeendelea kuonyesha ushindani mkali kati ya vigogo wa soka la Tanzania, Yanga SC na Azam FC, ambao tayari wamekutana mara mbili katika Ligi Kuu na Kombe la Muungano.
Katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana, kila moja ikijilinda na kupima nguvu za mpinzani wake. Hata hivyo, katika Kombe la Muungano, Yanga SC ilionyesha ubabe kwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Azam FC, matokeo yaliyowapeleka fainali ambayo hata hivyo walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya watani zao Simba .
Sasa bado kuna “dakika nyingine 180 za Derby ya Dar es salaam” timu hizo zikitarajiwa kukutana tena katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la CRDB. Mshindi wa pambano hilo atafuzu kwenda fainali kukutana na atakayeshinda kati ya Simba SC na Coastal Union
Aidha, safari yao bado haijaisha kabisa, kwani pia hawajakamilisha mechi ya duru ya pili ya Ligi Kuu ya NBC, ambapo Yanga SC watakuwa wenyeji wa Azam FC.
Mechi hizi mbili zinazotarajiwa kupigwa mwezi Juni 2026, zikitarajiwa kuwa mechi za kusisimua, zenye ushindani wa hali ya juu ambazo zinaweza kuamua hatma ya mataji kwa timu zote msimu huu.



