Safari ya timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana, kuelekea nchini Mexico kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 imekumbwa na changamoto baada ya kuchelewa kupatikana kwa visa za baadhi ya wachezaji na maafisa wa timu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka vyombo vya habari vya Afrika Kusini, safari ya timu hiyo ililazimika kuahirishwa kwa muda kutokana na matatizo ya nyaraka za kusafiria, hali iliyozua wasiwasi kwa mashabiki huku maandalizi ya michuano hiyo yakiendelea.
Bafana Bafana wanarejea kwenye Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010, ambapo walikuwa wenyeji wa mashindano hayo. Kocha Hugo Broos ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 26 kitakachowakilisha taifa hilo katika michuano itakayofanyika Marekani, Mexico na Canada.
Kikosi cha Wachezaji 26 wa Bafana Bafana
Makipa
Ronwen Williams (Mamelodi Sundowns)
Ricardo Goss (Siwelele)
Sipho Chaine (Orlando Pirates)
Mabeki
Khuliso Mudau
Aubrey Modiba
Khulumani Ndamane
Olwethu Makhanya
Bradley Cross
Thabang Matuludi
Nkosinathi Sibisi
Kamogelo Sebelebele
Ime Okon
Samukelo Kabini
Mbekezeli Mbokazi
Viungo
Teboho Mokoena
Jayden Adams
Thalente Mbatha
Sphephelo Sithole
Washambuliaji
Oswin Appollis
Tshepang Moremi
Evidence Makgopa
Relebohile Mofokeng
Lyle Foster
Iqraam Rayners
Themba Zwane
Thapelo Maseko
Kikosi hicho pia kinajumuisha nyota wawili ambao bado hawajacheza mechi yoyote ya kimataifa, Olwethu Makhanya na Bradley Cross, waliopata nafasi kutokana na ubora wao katika ngazi za klabu.
Mechi ya Kwanza Kombe la Dunia
Afrika Kusini itafungua kampeni yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo mkubwa dhidi ya wenyeji wenza wa mashindano hayo, Mexico, tarehe 11 Juni 2026 katika Uwanja wa Estadio Azteca mjini Mexico City.
Mchezo huo pia utakuwa wa ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026 na unatarajiwa kuvuta hisia kubwa kutokana na historia ya mataifa hayo mawili, yaliyokutana pia katika mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini.
Baada ya mechi dhidi ya Mexico, Bafana Bafana watacheza dhidi ya Czech Republic tarehe 18 Juni kabla ya kumaliza hatua ya makundi kwa kucheza na South Korea tarehe 24 Juni.



