Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne April 7 2026

Joel JJ By Joel JJ • 7th April 2026


Tetesi za usajili Ulaya, Jumanne April 7 2026

Soko la usajili linaendelea kupamba moto huku vilabu vikubwa vikianza kuchukua hatua za mapema kuhakikisha vinapata nyota wanaowahitaji. Hizi hapa ni tetesi kuu za leo barani Ulaya:


Liverpool Yapewa Nafasi kwa Camavinga

Liverpool wako katika nafasi nzuri ya kumsajili Eduardo Camavinga baada ya Real Madrid kuonyesha utayari wa kumuuza (L’Equipe).


Barcelona na Juventus Wamvizia Bernardo Silva

Barcelona na Juventus wanataka kumsajili Bernardo Silva kutoka Manchester City kwa uhamisho wa bure (Sky Sports).


Juventus Wamnyatia Ugarte

Juventus wanaamini kufuzu UEFA Champions League kutawasaidia kumsajili Manuel Ugarte kutoka Manchester United kwa takriban pauni milioni 35 (Corriere dello Sport).


Arsenal Wamzidi Liverpool kwa Diomande

Arsenal wanaonekana kuwa mbele ya Liverpool katika mbio za kumsajili Yan Diomande wa RB Leipzig (CaughtOffside).


Tottenham Wamwekea Bei Romero

Tottenham Hotspur hawako tayari kuuza Cristian Romero chini ya euro milioni 50, huku Atletico Madrid wakimhitaji (Fichajes).


Vinicius Jr: PSG au England?

Iwapo Vinicius Junior ataondoka Real Madrid, anaweza kujiunga na Paris Saint-Germain au klabu ya Premier League (ESPN).


Newcastle Wamfuatilia Coulibaly

Newcastle United wanapambana na vilabu vingine kumchukua Karim Coulibaly wa Werder Bremen (Fabrizio Romano).


Akliouche Awaniwa na United na Liverpool

Maghnes Akliouche wa AS Monaco anawindwa na Manchester United na Liverpool (TeamTalk).


Dortmund Wamfuatilia Diego Moreira

Borussia Dortmund wanamtaka Diego Moreira wa Strasbourg, lakini Chelsea wana kipengele cha kumnunua tena (Florian Plettenberg).


Roma Wawinda Vipaji Denmark

AS Roma wanawataka Dario Osorio na Franculino kutoka FC Midtjylland kwa dau la pamoja la euro milioni 55 (Gazzetta dello Sport).


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.