Soko la usajili linaendelea kushika kasi huku vilabu vikubwa vikifanya maamuzi muhimu kabla ya dirisha la majira ya kiangazi. Hizi hapa ni tetesi moto za leo kutoka vyanzo mbalimbali vya michezo:
Newcastle Wako Tayari Kumuza Anthony Gordon
Kwa mujibu wa The Times, Newcastle United wako tayari kumuuza Anthony Gordon kwenda Bayern Munich iwapo watapata ofa ya pauni milioni 75.
Manchester United Wamuwania Tchouameni
Ripoti kutoka The Telegraph zinaeleza kuwa Manchester United wanafuatilia kwa karibu hali ya Aurelien Tchouameni ndani ya Real Madrid, wakipanga kusajili viungo wawili msimu huu wa joto.
Liverpool Wamuweka Diomande Kama Mrithi wa Salah
Kwa mujibu wa Florian Plettenberg wa Sky Sport Germany, Liverpool FC wamemuweka Yan Diomande kama chaguo kuu la kuchukua nafasi ya Mohamed Salah.
Mustakabali wa Cristian Romero
CaughtOffside linaripoti kuwa Cristian Romero anawindwa na Atletico Madrid huku hatma yake ndani ya Tottenham Hotspur ikiwa haijulikani.
Curtis Jones Aweza Kuondoka Liverpool
Kwa mujibu wa Football Insider, Curtis Jones haridhishwi na muda mdogo wa kucheza ndani ya Liverpool na anaweza kuondoka majira ya joto.
Bastoni Aipendelea Barcelona
Ripoti kutoka Mundo Deportivo zinaeleza kuwa Alessandro Bastoni yuko tayari kuondoka Inter Milan lakini anaipendelea FC Barcelona kuliko Manchester City au Liverpool FC.
Liverpool Wamuwania Enzo Le Fee
Kwa mujibu wa Teamtalk, Liverpool FC ni miongoni mwa vilabu vinavyomuwania Enzo Le Fee kutoka Sunderland AFC.
Chelsea Wamwasiliana na Wakala wa Adeyemi
Ripoti za Fussballdaten zinaonyesha kuwa Chelsea FC wamewasiliana na wakala wa Karim Adeyemi wa Borussia Dortmund.
Everton Wamkaribia Hayden Hackney
Kwa mujibu wa Teamtalk, Everton FC wanaongoza mbio za kumsajili Hayden Hackney kutoka Middlesbrough FC.
John Stones Aweza Kuondoka Man City
Fabrizio Romano anaripoti kuwa John Stones anaweza kuondoka Manchester City kama mchezaji huru majira ya joto.



