Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi April 25 2026

Joel JJ By Joel JJ • 25th April 2026


Tetesi za usajili Ulaya, Jumamosi April 25 2026

Dirisha la usajili linazidi kupamba moto huku vilabu vikubwa Ulaya vikijipanga kwa ajili ya mabadiliko makubwa ya vikosi. Leo tunashuhudia majina mazito, dili kubwa zinazopikwa kimyakimya, na vita kali ya usajili kati ya miamba ya soka. Hizi hapa tetesi kuu za leo


Morgan Rogers awindwa na vigogo Ulaya

Kiungo mshambuliaji wa Aston Villa, Morgan Rogers (23), yuko tayari kujaribu maisha nje ya England.
Mabingwa wa Ulaya Paris Saint-Germain wameingia kwenye mbio hizo, wakishindana na:

  • Arsenal
  • Manchester United
  • Chelsea

Chanzo: Talksport


Manuel Akanji kuelekea Inter Milan

Beki wa Manchester City, Manuel Akanji, anatarajiwa kujiunga na Inter Milan kwa ada ya euro milioni 15.
Chanzo: Fabrizio Romano


City bado wanamng’ang’ania Elliot Anderson

Manchester City wana imani kubwa ya kumsajili Elliot Anderson kutoka Nottingham Forest kwa dau linaloweza kufikia pauni milioni 100.
Chanzo: The Sun


Lorenzo Lucca kurejea Napoli

Mshambuliaji Lorenzo Lucca atarejea Napoli baada ya mkopo wake kumalizika, huku Nottingham Forest wakikataa kumnunua moja kwa moja.
Chanzo: Corriere dello Sport


Real Madrid yaonyeshwa Bernardo Silva

Wakala maarufu Jorge Mendes amemuweka sokoni Bernardo Silva wa Manchester City kwa Real Madrid.
Mkataba wake unamalizika Juni 30.
Chanzo: AS


Joao Gomes kwenye rada ya Atletico

Atletico Madrid wameanza mazungumzo na Wolverhampton Wanderers kuhusu Joao Gomes.
Ada yake inaweza kufikia pauni milioni 40.
Chanzo: Talksport


Marcos Senesi karibu na Tottenham

Beki wa Argentina Marcos Senesi amekubaliana kimsingi kujiunga na Tottenham Hotspur akitokea AFC Bournemouth kwa uhamisho wa bure.
Chanzo: Florian Plettenberg


Manchester United bado wanamtaka Rafael Leao

Manchester United ni miongoni mwa wanaomfuatilia Rafael Leao wa AC Milan.
Chanzo: Calciomercato


Manchester City wamuweka tayari mrithi wa Guardiola

Kocha wa zamani wa Chelsea, Enzo Maresca, anatajwa kuwa chaguo la Manchester City endapo Pep Guardiola ataondoka.
Chanzo: Fabrizio Romano


Kalulu aingia kwenye rada ya United

Juventus wanataka kuongeza mkataba wa Pierre Kalulu, lakini Manchester United wanamfuatilia kwa karibu.
Chanzo: Tuttomercatoweb


Van de Ven ataka kuondoka Spurs

Beki Micky van de Ven hataki kuongeza mkataba wake na Tottenham Hotspur na anatafuta changamoto mpya.
Chanzo: Teamtalk


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.