Dirisha la usajili majira ya kiangazi linakaribia huku vilabu vikubwa vikianza kuweka wazi malengo yao. Leo, taarifa zinaonyesha harakati kubwa za kuimarisha vikosi, hasa katika Premier League.
Arsenal Waimarisha Ulinzi
Arsenal wanatafuta kuongeza nguvu safu ya ulinzi kwa kulenga kumsajili Victor Valdepenas wa Real Madrid pamoja na Jacobo Ramon wa Como (CaughtOffside).
Martinelli Ang’ang’ania Kubaki Arsenal
Gabriel Martinelli ameweka wazi nia yake ya kuendelea kusalia Arsenal licha ya tetesi za kuuzwa (Football Insider).
Dortmund Wamtaka Tena Jadon Sancho
Borussia Dortmund wanapanga jaribio la tatu kumsajili Jadon Sancho, ambaye yuko kwa mkopo Aston Villa kutoka Manchester United (Telegraph).
Tottenham Wamnyatia Trafford
Tottenham Hotspur wanamtaka James Trafford wa Manchester City kama sehemu ya mipango yao ya usajili (TeamTalk).
Ada Kubwa kwa Elliot Anderson
Nottingham Forest wanataka kati ya pauni milioni 100 hadi 120 kwa Elliot Anderson, anayewindwa na Manchester United na Manchester City (Florian Plettenberg).
Everton Wajaribu Kumuweka Grealish
Everton hawako tayari kulipa pauni milioni 50 kwa Jack Grealish, lakini wanataka kubaki naye kutoka Manchester City (The Athletic).
City Wamfuatilia Kijana Eichhorn
Manchester City wamejiunga na mbio za kumsajili chipukizi Kennet Eichhorn wa Hertha Berlin (Fabrizio Romano).
Leeds Wamruhusu Mateo Joseph Kuondoka
Leeds United wako tayari kumuuza Mateo Joseph baada ya mkopo wake Mallorca (Football Insider).
Chelsea Wamkingia Kifua Acheampong
Chelsea hawana mpango wa kumuuza Josh Acheampong licha ya kucheza mara chache (Express).
Garnacho Aingia Kwenye Radar ya River Plate
Kocha Eduardo Coudet wa River Plate amewasiliana na Chelsea na Alejandro Garnacho kuhusu uwezekano wa mkopo wa mwaka mmoja (TyC / Football London).



