TRA United yaizima Azam Fc Sheikh Amri Abeid

Joel JJ By Joel JJ β€’ 8th May 2026


TRA United yaizima Azam Fc Sheikh Amri Abeid

Azam Fc imepoteza mechi ya kwanza msimu huu baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya TRA United katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Zilikuwa dakika 90 ngumu kwa Azam Fc mbele ya vijan wa kocha Etienne Ndayiragieje ambao ushindi wa leo umewasogeza hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Azam Fc walikuwa wa kwanza kufunga bao la kuongoza dakika ya 7 kupitia kwa Jephte Kitambala hata hivyo TRA United walirejea mchezoni dakika ya 19 kwa bao la Ally Ng'anzi.

Ammy Mapaka akaongeza mabao mawili ya haraka haraka kabla ya mapumziko na Ramadhan Chobwedo kupigilia msumari wa mwisho dakika ya 64 kupitia mpira wa adhabu.

Kocha Florent Ibenge hakuamini kipigo hicho kwa kikosi chake baada ya dakika 90 kukamilika ukiwa mchezo wa kwanza kabisa Azam Fc wanapoteza msimu huu kwenye ligi.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.