TRA United yaichapa Pamba Jiji 1-0, yapanda nafasi ya 6

Joel JJ By Joel JJ β€’ 17th April 2026


TRA United yaichapa Pamba Jiji 1-0, yapanda nafasi ya 6

Klabu ya TRA United imeendelea kuonyesha makali yake nyumbani baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Pamba Jiji FC katika dimba la Sheikh Amri Abeid.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, Chanda Chewe akifunga bao pekee la ushindi katika dakika ya 60. Bao hilo lilitosha kabisa kuwapa TRA United alama tatu muhimu mbele ya mashabiki wao.

Pamba Jiji ilijaribu kusaka bao la kusawazisha kwa kushambulia mara kadhaa, lakini safu ya ulinzi ya TRA United ilikuwa imara na haikutoa nafasi rahisi hadi mwisho wa mchezo.

Kwa ushindi huo, TRA United imefikisha pointi 27 na kupanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kwa upande wa Pamba Jiji, kipigo hicho kimewaacha na pointi 26 na kushuka hadi nafasi ya saba, hali inayoongeza presha kwa wakulima hao wa Pamba katika mpango wao wa kusaka nafasi za juuu kwenye msimamo wa ligi.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.