Spurs yapata ushindi wa kwanza EPL 2026

Joel JJ By Joel JJ β€’ 25th April 2026


Spurs yapata ushindi wa kwanza EPL 2026

Klabu ya Tottenham Hotspur imepata ushindi wake wa kwanza mwaka 2026 katika Premier League baada ya kuichapa Wolverhampton Wanderers bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Jumamosi.

Bao pekee la mchezo huo lililofungwa na Palhinha lilitosha kuwapa Spurs pointi tatu muhimu, wakikatiza mfululizo wa matokeo mabaya uliokuwa umeiweka timu hiyo katika hatari kubwa ya kushuka daraja.

Licha ya ushindi huo, Tottenham bado inasalia katika nafasi ya 18 alama mbili nyuma ya West Ham kwenye msimamo wa ligi, ikihitaji matokeo mazuri zaidi katika michezo iliyobaki ili kujinusuru.

Katika mchezo mwingine, West Ham United iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Everton, katika pambano lililokuwa na ushindani mkali.

West Ham ilianza vyema kwa kupata bao la kuongoza kabla ya Everton kusawazisha, lakini bao la dakika za mwisho liliihakikishia ushindi huo muhimu wenyeji hao. Matokeo hayo yameiongezea West Ham matumaini ya kubaki ligi kuu, huku ikijinasua kidogo kutoka eneo la kushuka daraja.

Matokeo ya mechi nyingine, Fulham imeichapa Aston Villa bao 1-0 wakati Liverpool ikipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.