Wachezaji saba wa klabu ya Azam wameripotiwa kupata maumivu makali ya tumbo na kichwa ambapo wengi wao wamekimbizwa hospital ili kupatiwa matibabu.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa baadhi ya nyota wa kikosi hicho walionyesha dalili za kutokuwa sawa kiafya hali iliyowalazimu kupata uangalizi wa karibu kutoka kwa madaktari wa timu huku nyota Ashraf kibeku akidai alianza kuhisi vibaya mnamo dakika ya 20 wakati mechi yao na TRA inaendelea.
Wachezaji wengine ambao wameripotiwa kukumbwa na shida ya kiafya ni pamoja na Faisal Salum, Lusajo Mwaikenda na Pascal Msindo ambaye pia inaelezwa anapata shida kwenye kupumua na kooni kwake.
Hata hivyo hakuna taarifa rasmi kutoka uongozi wa Azam FC kuhusu chanzo cha hali hiyo wala ukubwa wa tatizo hilo.



