Singida BS, Simba viwanjani Muungano Cup Zanzibar

Joel JJ By Joel JJ • 23rd April 2026


Singida BS, Simba viwanjani Muungano Cup Zanzibar

Baada ya Yanga na Azam Fc kujihakikishia tiketi ya nusu fainali ya kombe la Muungano ambapo timu hizo zitaumana siku ya Jumamosi, leo mechi nyingine za robo fainali zitapigwa kuamua mechi ya pili ya nusu fainali.

Mapema saa 10:15 jioni, Mlandege watakuwa wenyeji wa Singida BS mchezo utakaopigwa uwanja wa New Amaan Complex.

Je Mlandege wataweza kuizuia Singida BS na kuwa timu ya kwanza kutoka visiwani Zanzibar kufuzu nusu fainali?

Mchezo utakaofuata ni kati ya Simba dhidi ya Mafunzo Fc utakaopigwa saa 2:15 usiku. 

Baada ya watani zao Yanga kufuzu nusu fainali ni wazi Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo la kufuzu hatua inayofuata.

Washindi wa mechi hizo watakutana kwenye hatua ya nusu fainali.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.