Simba yahusishwa na kiungo Marumo Gallants

Joel JJ By Joel JJ β€’ 6th May 2026


Simba yahusishwa na kiungo Marumo Gallants

Klabu ya Simba SC inatajwa kuingia kwenye mazungumzo ya kumuwania kiungo mkabaji Ibrahim Bance kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini.

Kiungo huyo raia wa Burkina Faso anatajwa kuwa chaguo la kocha wa Simba, Steve Barker, ambaye anaamini ataongeza nguvu katika eneo la kiungo mkabaji ndani ya timu hiyo.

Barker anatafuta mbadala sahihi wa Allasane Kante, ambaye ameripotiwa huenda akapewa mkono wa kwaheri mwishoni mwa msimu.

Taarifa zinaeleza kuwa Bance anatarajiwa kumaliza mkataba wake na Marumo Gallants mwishoni mwa msimu huu, hali inayofungua mlango kwa Simba kumpata bila gharama kubwa akiwa kama mchezaji huru.

Iwapo mazungumzo hayo yatafanikiwa, basi Simba itakuwa imepata kiungo mwenye uwezo wa kukaba, kusoma mchezo na kusaidia ujenzi wa mashambulizi kutoka chini akishirikiana na viungo wengine.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.