Klabu ya Simba imetangaza kuhamia uwanja wa KMC Complex na kwamba mechi za msimu huu zilizobaki zitapigwa katika uwanja huo.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imebainisha kuwa hali ya hewa ya mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es salaam ni moja ya sababu iliyopelekea uamuzi huo
“Kutokana na hali ya hewa ya mvua kuendelea kunyesha jijini Dar es Salaam kikosi chetu kimerejea kucheza mechi za nyumbani katika Uwanja wa KMC Complex”
“Hii ina maana kuwa mechi zetu zilizosalia zamsimu wa Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 ambazo tutakuwa nyumbani tutacheza katika Uwanja wa KMC Complex”
“Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons utapigwa Jumapili Mei 10 utakuwa wa kwanza kupigwa katika Uwanjawa KMC Complex,” ilibainisha taarifa ya Simba



