Simba kwenda Arusha kwa mafungu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 6th April 2026


Simba kwenda Arusha kwa mafungu

Baadhi ya wachezaji wa Simba usiku wa leo wataondoka jijini Dar es salaam kuelekea Arusha wanakokabiliwa na mfululizo wa mechi za ligi kuu ya kombe la CRDB.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema msafara wa kwanza utaondoka saa 8 usiku na msafara wa pili kuondoka kesho saa 12 asubuhi.

Simba inakabiliwa na mechi tatu jijini Arusha ambao zote zitapigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

April 09 watacheza dhidi ya TRA United, April 12 watacheza dhidi ya Dodoma Jiji (kombe la CRDB) na April 15 watacheza dhidi ya Fountain Gate.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.