SAMATTA AENDELEA KUWEKA REKODI ULAYA, AFUNGA BAO LA KWANZA LE HAVRE LIGUE 1

Joel JJ By Joel JJ β€’ 13th April 2026


SAMATTA AENDELEA KUWEKA REKODI ULAYA, AFUNGA BAO LA KWANZA LE HAVRE LIGUE 1

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, ameendelea kuandika historia barani Ulaya baada ya kufunga bao lake la kwanza akiwa na klabu ya Le Havre AC katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Samatta alifunga bao hilo jana Jumapili, Aprili 12, 2026, katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya OGC Nice, uliochezwa katika Uwanja wa Allianz Riviera. Nyota huyo wa Tanzania alifunga dakika ya 41 baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa kiungo Rassoul Ndiaye.

Bao hilo ni la kwanza kwa Samatta tangu ajiunge na Le Havre katika dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi, na linakuja baada ya kipindi cha wiki kadhaa bila kufunga kwa klabu hiyo mpya.

Takwimu zinaonyesha kuwa wiki tatu kabla ya mchezo huo, Samatta alitoa mchango wa pasi ya bao katika mchezo wa Ligue 1 dhidi ya Paris FC, ambapo Le Havre ilipoteza kwa mabao 3-2.

Kwa kufunga katika Ligue 1, Samatta sasa ameendelea kuimarisha rekodi yake ya kipekee barani Ulaya kwa kufunga katika ligi tano tofauti, ambazo ni Ligi Kuu England (EPL), Ligi Kuu ya Ubelgiji, Ligi Kuu ya Uturuki, Ligi Kuu ya Ugiriki na sasa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Takwimu zinamweka Samatta miongoni mwa wachezaji wachache wa Afrika Mashariki walioweza kufanya vizuri katika ligi mbalimbali kubwa za Ulaya.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.