Ligi Kuu ya NBC inazidi kuchanja mbuga ikiingia mzunguuko wa 24 ambapo mechi nane zinatarajiwa kupigwa katika viwanja tofauti.
Katika hatua hii vita kubwa iko juu ya msimamo klabu za Yanga, Simba na Azam Fc zikichuana kwenye mbio za ubingwa.
Lakini pia chini ya msimamo kuna vita ya aina yake, KMC, Tanzania Prisons, Mbeya City, Fountain Gate, Coastal Union na nyingine zikichuana kuepuka shimo la kushuka daraja.
Dalili sio nzuri kwa KMC ambao ni kama wameshakata tiketi ya kucheza Championship msimu ujao huku Tanzania Prisons nao wakionyesha dalila ya kuungana nao.
Vita kubwa bado ipo kwenye eneo la kucheza play-off ya kushuka/kusalia ligi kuu
Hii hapa ratiba ya mechi zote za raundi ya 24




