Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha mchezo wa nusu fainali ya kombe la CRDB kati ya Simba dhidi ya Coastal Union utapigwa Juni 20, 2026.
Mtanange huo umepangwa kupigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Juni 21 itapigwa nusu fainali ya pili kati ya Azam Fc dhidi ya Yanga mchezo utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.




