Michuano ya kombe la Muungano inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumanne, April 21 ratiba ya michuano hiyo ikiwekwa hadharani leo.
Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga watashuka dimbani Jumanne kumenyana na M/Makumbi mchezo utakaopigwa saa 1:15 usiku.
Kama Yanga itatinga nusu fainali, katika hatua hiyo itakutana na mshindi wa mchezo kati ya KVZ dhidi ya Azam Fc.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Simba itashuka dimbani Alhamisi, April 23 kuikabili Mafunzo Fc mchezo utakaopigwa saa 2:15 usiku.
Endapo Simba itavuka hatua hiyo, nusu fainali itacheza na mshindi kati ya Mlandege Fc dhidi ya Singida BS.
Hii hapa ratiba kamili;




