Klabu ya Singida BS imemuajiri aliyekuwa kocha wa Maniema Union Papy Kimoto kuwa Meneja Mkuu huku wakimtangaza Kapiten Ngoy Dora kuwa kocha msaidizi.
Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Singida BS mapema Ijumaa, nafasi ya Kocha Mkuu itaendelea kuwa chini ya Muhibu Kanu hadi mwishoni mwa msimu.




