Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez, ameripotiwa kuanza jitihada za kumrejesha kocha Jose Mourinho kuinoa timu hiyo kuelekea msimu ujao.
Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, Perez anadaiwa kumtazama Mourinho kama chaguo kuu la kuiongoza timu hiyo, huku klabu hiyo ikifikiria kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi baada ya msimu usioridhisha.
Inaelezwa kuwa rais huyo anaamini uzoefu na uwezo wa Mourinho katika mashindano makubwa unaweza kusaidia kurejesha ushindani na nidhamu ndani ya kikosi cha Real Madrid.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa ndani ya uongozi wa klabu hiyo kuna mitazamo tofauti kuhusu uamuzi huo, ambapo baadhi ya viongozi wanapendelea makocha wa kizazi kipya wenye falsafa ya muda mrefu.
Jose Mourinho aliwahi kuinoa Real Madrid kati ya mwaka 2010 na 2013, ambapo alifanikiwa kuipa taji la La Liga pamoja na kuvunja rekodi ya pointi 100 katika msimu mmoja.



