PSG, Atletico mguu ndani nusu fainali UEFA.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 9th April 2026


PSG, Atletico mguu ndani nusu fainali UEFA.

Matokeo ya michezo ya leo ya UEFA Champions League yameendelea kuonyesha ushindani mkali katika hatua ya robo fainali mzunguko wa kwanza:

• Barcelona 0–2 Atlético Madrid

Barcelona wakiwa nyumbani wamechezea kichapo cha magoli mawili kwa bila mchezo huo huku wakilazimika kucheza pungufu kufuatia kadi nyekundu aliyoipata beki wao Pau Cubarsí. Mabao ya Julián Álvarez na Alexander Sørloth yaliihakikishia Atlético Madrid ushindi muhimu ugenini.

• Paris Saint-Germain 2–0 Liverpool

PSG nao wameendelea kuonyesha ubora wao wakiwa nyumbani kwa kuibuka na ushindi mzuri dhidi ya Liverpool. Mabao ya Désiré Doué na Khvicha Kvaratskhelia yalitosha kuwapa faida muhimu kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa katika dimba la Anfield ( uingereza).

Matokeo haya yanaweka presha kubwa kwa Barcelona na Liverpool katika michezo ijayo, huku Atlético Madrid na PSG wakijijengea nafasi nzuri ya kusonga mbele.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.