Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Shadrack Nsajigwa bado anaendelea kusaka ushindi wake wa kwanza katika Ligi Kuu NBC Tanzania Bara tangu ajiunge na kikosi hicho.
Nsajigwa ambaye aliwahi kuwa nahodha wa Yanga ameiongoza Tanzania Prisons katika michezo tisa ya ligi kuu bila kupata ushindi hata mmoja, hali inayozidi kuongeza presha ndani ya timu hiyo.
Katika mechi hizo tisa, Prisons imefanikiwa kupata sare mbili pekee huku ikipoteza michezo saba.
Matokeo ya Tanzania Prisons chini ya Nsajigwa yamekuwa kama ifuatavyo:
- 0-0 dhidi ya Azam FC
- 0-1 dhidi ya Yanga
- 1-2 dhidi ya Singida Black Stars
- 0-1 dhidi ya TMA Stars
- 0-3 dhidi ya Yanga
- 1-1 dhidi ya KMC FC
- 0-3 dhidi ya TRA United
- 1-2 dhidi ya Mbeya City FC
- 0-4 dhidi ya Simba SC
Matokeo hayo yanaifanya Tanzania Prisons kuendelea kuwa kwenye wakati mgumu ikisalia kwenye nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 14 tu.



