Ni Tanzania dhidi ya Senegal fainali Afcon U17 leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 2nd June 2026


Ni Tanzania dhidi ya Senegal fainali Afcon U17 leo

Macho ya mashabiki wa soka Tanzania na Afrika kwa ujumla leo yataelekezwa jijini Rabat, Morocco, ambapo Serengeti Boys watachuana na Senegal katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 (AFCON U-17) 2026.

Mchezo huo wa kihistoria utapigwa kwenye Uwanja wa Moulay El Hassan kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania.

Tanzania imefika fainali ya mashindano haya kwa mara ya kwanza katika historia yake baada ya kuiondoa Misri kwa mikwaju ya penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana katika hatua ya nusu fainali. Mafanikio hayo yanaendelea kuthibitisha ukuaji mkubwa wa soka la vijana nchini, hasa baada ya mafanikio ya Tanzania katika Mashindano ya Shule za Afrika ya CAF katika miaka ya karibuni.

Safari ya Serengeti Boys imekuwa ya kuvutia, huku vijana hao wakionyesha nidhamu, umoja na uwezo mkubwa wa kupambana katika kila hatua ya mashindano.

Upande wa Senegal nao wameonyesha ubora wao kwa kufika fainali baada ya kuiondoa Morocco wenyeji wa mashindano kwa mikwaju ya penalti 7-6 kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo wa nusu fainali.

Moja ya silaha kubwa za Senegal ni kipa na nahodha wao, Assane Sarr, ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika safari ya timu hiyo kuelekea fainali. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 16 ameonekana kuwa nguzo muhimu ya safu ya ulinzi ya Senegal katika mechi za mtoano.

Mechi ya Fahari kwa Afrika Mashariki

Kwa Tanzania, ushindi leo utamaanisha kutwaa ubingwa wa AFCON U-17 kwa mara ya kwanza kabisa. Kwa Senegal, ushindi utaendelea kuimarisha hadhi yao kama moja ya mataifa yenye mfumo bora wa kuibua vipaji vya soka barani Afrika.Senegal ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo

Tayari timu zote mbili zimefuzu kushiriki Kombe la Dunia la FIFA kwa vijana chini ya miaka 17 litakalofanyika Qatar baadaye mwaka huu, lakini fainali ya leo itakuwa vita ya heshima na ubingwa wa Afrika.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.