Mudathir afungiwa, Kamati ya saa 72 yatembeza faini

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th April 2026


Mudathir afungiwa, Kamati ya saa 72 yatembeza faini

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kupitia Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha tarehe 18 Aprili, 2026, kuhusu matukio mbalimbali ya Ligi na maamuzi yaliyofikiwa:

Maamuzi ya Ligi Kuu ya NBC

1. Mechi Namba 07: TRA United FC 0-0 Simba SC

  • Adhabu: Vilabu vya TRA United na Simba SC vimetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kila kimoja.

  • Kosa: Walinzi wa klabu hizo (Stewards) kupigana mara baada ya timu kuwasili kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

  • Kanuni: 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

2. Mechi Namba 132: Pamba Jiji FC 0-3 Young Africans SC

  • Adhabu: Mchezaji Mudathir Yahya (Young Africans) amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja).

  • Kosa: Kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji, Ibrahim Abraham, mchezo ukiwa unaendelea kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

  • Kanuni: 41:5(5.2) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

3. Mechi Namba 146: Coastal Union FC 1-1 Mtibwa Sugar FC

  • Adhabu: Klabu ya Coastal Union imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano).

  • Kosa: Mashabiki wake kurusha chupa za maji uwanjani wakati waamuzi wakiwatuliza Victor Collins (Mtibwa Sugar) na Athuman Makambo (Coastal Union) baada ya Victor kumsukuma Makambo.

  • Kanuni: 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

4. Mechi Namba 151: TRA United 2-0 Singida BS

  • Adhabu: Klabu ya Singida BS imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano).

  • Kosa: Viongozi wake wawili kuingia uwanjani na kumwaga viminimika, jambo lililotafsiriwa kama imani za kishirikina kabla ya timu kupasha moto misuli.

  • Kanuni: 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

5. Mechi Namba 152: Azam FC 0-0 Simba SC

  • Adhabu kwa Azam FC: Imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano).

    • Kosa: Viongozi wa benchi la ufundi na wachezaji kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani kinyume na kanuni na makubaliano ya kikao cha maandalizi (Pre-match meeting).

    • Kanuni: 17:21 na 17:62 kuhusu Taratibu za Mchezo.

  • Adhabu kwa Simba SC: Imetozwa faini ya Sh. 10,000,000 (milioni kumi).

    • Kosa: Mashabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi namba mbili baada ya kuonyesha kibendera kuashiria mchezaji wa Simba ameotea (offside).

    • Maelezo ya ziada: Hili ni kosa la kujirudia kwa klabu ya Simba msimu huu (2025/2026), ambapo mashabiki walishafanya kosa kama hilo katika michezo miwili tofauti awali.

    • Kanuni: 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.