Ripoti mpya kutoka vyanzo vya soka barani Ulaya zinaeleza kuwa kocha mtarajiwa wa Real Madrid José Mourinho amepitisha usajili wa beki wa Liverpool Ibrahima Konaté pamoja na beki wa pembeni wa Inter Milan Denzel Dumfries kujiunga na miamba hiyo ya Hispania baada ya mchakato wa uchaguzi wa uongozi ndani ya klabu kukamilika.
Inaelezwa kuwa tayari kuna mazungumzo ya awali yaliyofanyika na pande husika, na hata makubaliano ya maneno (verbal agreements) yanadaiwa kufikiwa kwa baadhi ya vipengele vya usajili.
Kwa mujibu wa nguli wa habari za usajili Fabrizio Romano, nyota hao watajiunga na Real Madrid baada ya taratibu za uchaguzi ndani ya klabu hiyo kukamilika.
Mourinho ameanza kwa kuisuka upya safu ya ulinzi. Konaté anatajwa kwa uwezo wake eneo la beki wa kati, uongozi na nguvu katika kuzuia mashambulizi, huku Dumfries akiwa na kasi na mchango mkubwa katika kushambulia kutoka pembeni.



