Mnyama kuzisaka alama tatu dhidi ya Prisons, mechi tatu ligi kuu leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 10th May 2026


Mnyama kuzisaka alama tatu dhidi ya Prisons, mechi tatu ligi kuu leo

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo mzunguuko wa 22 ambapo mechi tatu zinatarajiwa kupigwa katika viwanja tofauti.

Mchezo wa mapema saa 8, KMC watakuwa wenyeji wa Fountain Gate katika mchezo ambao watoza ushuru hao wanahitaji kushinda wakitegemea muujiza wa kunusurika kushuka daraja.

Pamba Jiji itakuwa mwenyeji wa Dodoma Jiji katika mchezo utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba kabla ya Simba kuikaribisha Tanzania Prisons katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku dimba la KMC Complex.

Simba inahitaji ushindi ili kuendelea kuwa na matumaini kwenye mbio za ubingwa wakati Prisons wanahitaji ushindi kujiondoa kwenye eneo la hatari kushuka daraja.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.