Klabu y Fountain Gate imemtangaza Fredy Felix Minziro kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo akisaidiwa na Makocha Wasaidizi Mathias Wandiba na Aboubakar Francis.
Minziro amejiunga na Fountain Gate akichukua nafasi ya aliyekuwa Kocha Mkuu Mohamed Laizer ambaye ameondoka kunako klabu hiyo kwa makubaliano ya pande mbili.




