Michael Olise atwaa tuzo ya mchezaji bora Bundesliga 2025/26

Joel JJ By Joel JJ β€’ 17th May 2026


Michael Olise atwaa tuzo ya mchezaji bora Bundesliga 2025/26

Nyota wa FC Bayern Munich na timu ya taifa ya France, Michael Olise, ametangazwa rasmi kuwa Mchezaji Bora wa Bundesliga msimu wa 2025/26 akiwa na umri wa miaka 24.

Olise alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi katika safari ya Bayern Munich kutwaa ubingwa wa Bundesliga msimu huu. Winga huyo wa kushoto alimaliza ligi akiwa na mabao 15 na assists 19 ndani ya mechi 32 takwimu zilizomfanya kuwa mmoja wa wachezaji hatari zaidi Ulaya kwa sasa.

Kwa mujibu wa Bundesliga, viongozi wa DFL Marc Lenz na Steffen Merkel walimkabidhi tuzo hiyo muda mfupi kabla ya Bayern Munich kukabidhiwa kombe la Bundesliga katika dimba la Allianz Arena.

Msimu wa Kihistoria kwa Olise

Michael Olise ameendelea kuthibitisha kuwa ni mmoja wa mawinga bora duniani tangu ajiunge na Bayern Munich akitokea Crystal Palace F.C. mwaka 2024. Ndani ya misimu miwili pekee nchini Ujerumani, tayari ameshinda:

  • Bundesliga mara mbili
  • Tuzo ya Rookie of the Season 2024/25
  • Player of the Season 2025/26
  • Tuzo kadhaa za Player of the Month Bundesliga

Wachambuzi wa soka nchini Ujerumani wamemlinganisha Olise na gwiji wa zamani wa Bayern, Arjen Robben, kutokana na uwezo wake wa kupenya upande wa kulia, kasi, ubunifu na umaliziaji wake wa hali ya juu.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.