Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo mechi za mzunguuko wa 24 zikiendelea kupigwa katika viwanja mbalimbali.
Dimba la Isamuhyo wenyeji JKT Tanzania watawakariisha Fountain Gate mchezo utakaopigwa saa 10 jioni.
JKT Tanzania iko kwenye mapambano ya kuwania tiketi ya kushiriki mashindano ya CAF msimu ujao hivyo ni mchezo ambao wanahitaji kushinda.
Mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini ni kati ya Coastal Union dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Ni mchezo ambao kama Simba itaibuka na ushindi, itapanda kileleni mwa msimamo wa ligi angalau kwa saa 24 kabla ya watani zao Yanga kushuka dimbani kukabiliana na Sngida BS hapo kesho.
Hata hivyo Coastal Union nao hawako kwenye eneo salama katika msimamo wa ligi hivyo ni mchezo ambao ushindi au hata matokeo ya sare yatakuwa na maana kubwa kwao.
Namungo Fc na Mbeya City watahitimisha mchezo wa mwisho leo utakaopigwa saa 3 usiku uwanja wa Majaliwa.




