Mamlaka za soka nchini Morocco zimesitisha mechi zote za kirafiki zilizokuwa zimepangwa kuchezwa na timu za mataifa mbalimbali zilizoko nchini humo, kufuatia tahadhari mpya za kiafya.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo, uamuzi huo umechukuliwa kutokana na hofu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, hali iliyosababisha mamlaka kuchukua hatua za haraka za kinga.
Hatua hiyo imeathiri mipango ya maandalizi ya timu kadhaa za taifa ambazo zilikuwa zipo Morocco kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa.
Miongoni mwa timu zilizoathirika na uamuzi huo ni Tanzania, ambayo iliwahi kuwasili nchini humo jana kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Uganda na Rwanda.



