Klabu ya Mbeya City imemfuta kazi Kocha Meckie Mexime na makocha wasaidizi baada ya kipigo cha mabao 6-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Hicho kilikuwa kipigo 'kizito' cha pili mfululizo baada ya kuvurumishwa mabao 5-1 na Singida BS kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la CRDB.




