Mbappe Atarajia Presha Kubwa Real Madrid Kabla ya Mtanange na Bayern Munich

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media β€’ 7th April 2026


Mbappe Atarajia Presha Kubwa Real Madrid Kabla ya Mtanange na Bayern Munich

Shinikizo linaendelea kumwandama mshambuliaji nyota Kylian Mbappé kuelekea mchezo mkubwa wa robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Bayern Munich.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka MARCA, baadhi ya mashabiki wa Real Madrid katika dimba la Santiago Bernabéu wanatajwa kuwa tayari kuonyesha kutoridhishwa kwao endapo Mbappé hatatoa kiwango kinachotarajiwa katika mchezo huo wa leo.

Inaripotiwa kuwa hali ya kupigiwa kelele na kuzomewa inaweza kujitokeza iwapo mshambuliaji huyo hatakuwa na mchango mkubwa uwanjani.

Shinikizo la aina hii si jambo geni ndani ya klabu hiyo, ambayo inajulikana kwa viwango vya juu vya matarajio kwa wachezaji wake. Historia inaonyesha kuwa hata majina makubwa kama Zinedine Zidane, Ronaldo Nazário na Cristiano Ronaldo waliwahi kukumbana na hali kama hiyo katika vipindi tofauti walipokuwa klabuni hapo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.