Siku ya leo Jumapili kuna mechi kadhaa za Premia zinapigwa lakini mechi inayoangaziwa na wengi ni ile kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool na ule kati ya Aston Villa dhidi ya Tottenham iliyo kwenye vita ya kujinusuru kuteremka daraja.
Man United vs Liverpool β Dabi ya kihistoria Old Trafford
Katika mchezo mkubwa zaidi wa siku, Manchester United wanawakaribisha Liverpool FC katika pambano linalobeba uzito wa nafasi za juu za ligi, saa 11:30 jioni.
Mechi hii, ambayo ni mojawapo ya dabi maarufu duniani, inaathiri moja kwa moja vita ya kumaliza ndani ya nafasi nne za juu. Liverpool wanahitaji ushindi ili kuendelea kuweka matumaini ya kufuzu UEFA Champions League, wakati Manchester United wakilenga kuimarisha nafasi yao ya juu katika msimamo wa ligi.
Ushindani kati ya timu hizi mbili unatarajiwa kuwa mkali kutokana na historia yao ndefu ya upinzani na presha ya msimu wa mwisho.
Aston Villa vs Tottenham Hotspur β Vita ya Ulaya Villa Park
Katika dimba la Villa Park, Aston Villa wanawakaribisha Tottenham Hotspur katika mchezo muhimu unaogusa moja kwa moja vita mbili tofauti.
Aston Villa wanapigania kujiweka katika nafasi za juu za msimamo ili kujihakikishia tiketi ya kuchez mashindano ya UEFA, huku Tottenham wakihitaji matokeo ili kuendelea na mapambano ya kujinusuru kushuka daraja.
Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa kasi na wenye ushindani mkubwa kutokana na malengo tofauti lakini muhimu kwa pande zote mbili.
Bournemouth vs Crystal Palace β Mapambano ya katikati ya msimamo
Katika mchezo mwingine wa siku, AFC Bournemouth wanacheza dhidi ya Crystal Palace FC katika mchezo unaolenga kujihakikishia usalama wa katikati ya jedwali.
Ingawa hauko kwenye mvuto wa ubingwa au nafasi za juu, mchezo huu una umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili kuhakikisha hazishuki zaidi kwenye msimamo.



