Manchester City yaiondoa Arsenal kileleni baada ya siku 200

Joel JJ By Joel JJ • 23rd April 2026


Manchester City yaiondoa Arsenal kileleni baada ya siku 200

Mabingwa watetezi Manchester City wamefanikiwa kuiondoa Arsenal kileleni mwa msimamo wa Premier League baada ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Burnley katika mchezo uliopigwa Jumatano usiku.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa mapema na mshambuliaji nyota Erling Haaland, bao ambalo lilitosha kabisa kuwapa pointi tatu muhimu na kuipandisha City kileleni mwa msimamo wa ligi.

Matokeo hayo yana umuhimu mkubwa kwani yamekatiza rekodi ya Arsenal iliyokuwa imekaa kileleni kwa takribani siku 200 mfululizo, kabla ya kushushwa na wapinzani wao hao wakubwa katika mbio za ubingwa. 

Mbali na hilo, ushindi huo pia umehitimisha rasmi safari ya Burnley katika ligi hiyo, baada ya kuthibitishwa kushuka daraja kufuatia kupoteza mchezo huo muhimu. 

Manchester City sasa wanaongoza msimamo wakiwa na pointi 70 sawa na Arsenal lakini wakizidi kwa idadi ya mabao ya kufunga, jambo linalofanya mbio za ubingwa kuwa kali zaidi kuelekea mwisho wa msimu.

Hii inaashiria kurejea kwa nguvu kwa kikosi cha City chini ya kocha Pep Guardiola, huku Arsenal wakilazimika kupambana zaidi ili kurejesha nafasi yao ya juu.

Je, Manchester City wataendelea kubaki kileleni hadi mwisho wa msimu, au Arsenal watarejea kwa nguvu?


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.