Manchester City wameendelea kuonyesha dhamira ya kweli ya kuwania ubingwa baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa ligi uliopigwa darajani.
Katika mchezo huo, City walikuwa bora kuanzia mwanzo hadi mwisho, wakitawala umiliki wa mpira na kutengeneza nafasi nyingi za mabao. Nico O’Reilly aliifungia City bao la kwanza, kabla ya Guehi kuongeza la pili na kuifanya timu hiyo kuwa katika nafasi nzuri zaidi. Jeremy Doku alihitimisha ushindi huo kwa bao la tatu, akihakikisha alama zote tatu zinakwenda upande wa Pep Guardiola.
Matokeo hayo yanazidi kuwapa nguvu Manchester City katika mbio za ubingwa, huku wakipunguza pengo la pointi dhidi ya vinara wa ligi na kuongeza presha katika hatua za mwisho za msimu.



