Makocha Yanga, Namungo Fc wafunguka

Joel JJ By Joel JJ • 24th May 2026


Makocha Yanga, Namungo Fc wafunguka

Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moalin, ametoa ujumbe mzito kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC utakaopigwa kesho Jumatatu katika Uwanja wa KMC Complex, akisisitiza kuwa kikosi chake kipo tayari licha ya muda mfupi wa maandalizi.

Moalin amesema kuwa wachezaji wake wanaelewa umuhimu wa mchezo huo na malengo yao ni kuendelea kukusanya pointi tatu tatu bila kuangalia ubora wa wapinzani wao.

Amesema:

“Maandalizi ya mchezo wetu wa kesho dhidi ya Namungo yanaendelea vizuri, tuna muda mchache lakini tuna matumaini makubwa. Namungo ni timu ngumu lakini kipaumbele chetu ni alama tatu…”

“Tunatambua umuhimu wa kila mchezo, hatuogopi kufanya kazi katika mazingira yenye presha. Tunacheza kama tunavyocheza siku zote, sisi ni Yanga. Tunahitaji presha ili kutusukuma mbele zaidi…”

“Kila mchezaji anajua mashabiki na timu inataka nini… Pacome alipata majeraha kidogo mchezo uliopita lakini anaendelea vizuri… tunahitaji hamasa ya kutosha kutoka kwa mashabiki.”

Mgunda Ajibu: Tunalenga Ushindi Dhidi ya Yanga

Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu wa Namungo FC, Juma Mgunda amesema timu yake imejiandaa vizuri kucheza soka la ushindi dhidi ya mabingwa hao watetezi, akisisitiza kuwa wanahitaji alama tatu muhimu ili kupanda kwenye msimamo wa ligi.

Mgunda amesema mchezo huo hautakuwa rahisi, lakini wachezaji wake wako tayari kupambana kupata matokeo chanya.

Amesema:

“Tumejiandaa kucheza mchezo mzuri dhidi ya timu nzuri ya Yanga. Hautakuwa mchezo rahisi kwa sababu wao wanahitaji alama tatu na sisi tunahitaji alama tatu pia ili tusogee kutoka hapa tulipo…”


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.