Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo mzunguuko wa 21 ambapo mechi tatu zinatarajiwa kupigwa katika viwanja mbalimbali.
Katika uwanja wa Airtel, Mtipa mkoani Singida, wenyeji Singida BS wataikaribisha Pamba Jiji katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Pamba Jiji wako kwenye kiwango bora wakitoka kupata ushindi ugenini dhidi ya Fountain Gate wakati Singida BS wakipoteza mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union.
Fountain Gate na Coastal Union nazo zitachuana katika mchezo utakaopigwa majira ya saa 10:15 jioni huku Azam Fc wakitarajiwa kuchuana na Namungo Fc katika mchezo mwingine.




