Ligi Kuu ya NBC May 13, mechi mbili kupigwa leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 13th May 2026


Ligi Kuu ya NBC May 13, mechi mbili kupigwa leo

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo mzunguuko wa 23 ambapo mechi mbili zinatarajiwa kupigwa.

Mchezo wa mapema saa nane mchana, Mbeya City wataikaribisha Coastal Union katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine.

Ni wazi Mbeya City wanahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja.

Mchezo unosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka ni kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Yanga utakaopigwa saa 10 jioni kwenye uwanja wa Airtel Mtipa mkoani Singida.

Dodoma Jiji ni wenyeji wa mchezo huo lakini unapigwa mkoani Singida kutokana na kufungiwa kwa uwanja wa Jamhuri.

Ushindi kwa Yanga utazidi kuwaweka Wananchi katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wakati alama tatu kwa Dodoma Jiji itawaweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.