Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo ratiba ya mechi za raundi ya 25, mechi nne zinatarajiwa kupigwa.
Saa 10 jioni TRA United wataikaribisha Fountain Gate mchezo utakaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid huku mchezo kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya JKT Tanzania nao iikipigwa katika muda huo uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Saa 12:15 mechi inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini kati ya Simba dhidi ya Dodoma Jiji itapigwa uwanja wa KMC Complex.
Simba itarudi kileleni mwa msimamo wa ligi kama itashinda mchezo huo huku Dodoma Jiji wakipania kuchukua alama tatu nyingine mitaa ya Kariakoo baada ya ushindi dhidi ya Yanga.
Coastal Union watachuana na Mashujaa Fc katika mchezo wa mwisho siku ya leo utakaopigwa saa 2:30 usiku uwanja wa Mkwakwani.




