Ligi Kuu kuendelea leo, mechi mbili za kuhitimisha mzunguuko wa 25

Joel JJ By Joel JJ β€’ 26th May 2026


Ligi Kuu kuendelea leo, mechi mbili za kuhitimisha mzunguuko wa 25

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi mbili za kuhitimisha mzunguuko wa 25 zinatarajiwa kupigwa.

Mapema saa 8 Pamba Jiji itashuka dimba la CCM Kirumba kuikabili tanzania Prisons katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Prisons wako eneo la kushuka daraja, pengine wanahitaji kuanza kukusanya pointi kabla ya kupoteza matumaini.

Singida BS na Mbeya City zitachuana katika mchezo mwingine utakaopigwa saa 10 jioni.

Singida BS wanahitaji ushindi ili kujiimarisha kwenye nafasi ya nne wakati Mbeya City watahitaji ushindi ili kusogea juu kutoka eneo la kucheza play-off.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.