Baada ya kuhitimishwa kwa michuano ya kombe la Muungano jana Simba wakiibuka mabingwa kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao Yanga katika mchezo wa fainali uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar, mikiki ya ligi kuu ya NBC inarejea leo mechi za raundi ya 20 zikianza.
Mchezo wa mapema, Fountain Gate wataikaribisha Pamba Jiji katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, saa 8 mchana.
Mbeya City watakuwa wenyeji wa Mashujaa Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine saa 10:15 ukiwa ni mchezo wa kwanza tangu kufunguliwa kwa dimba la Sokoine.
Dimba la KMC Complex, utapigwa mchezo mwingine ambapo JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa KMC mchezo utakaopigwa saa 12:30 jion.




