Ligi Kuu NBC, May 25 mechi mbili kupigwa leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 25th May 2026


Ligi Kuu NBC, May 25 mechi mbili kupigwa leo

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo zikiwa ni mechi za kukamilisha mzunguuko wa 25.

Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watakuwa uwanja wa KMC Complex kuikabili Namungo Fc katika mechi inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Yanga inahitaji ushindi ili kurejea juu ya msimamo wakati Namungo Fc wanapambana kujiweka salama kuepuka hatari ya kushuka daraja wakicheza takribani mechi 13 bila kupata ushindi kwenye ligi.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 12:30 jioni na kisha siku kuhitimishwa na mchezo kati ya Azam Fc dhidi ya KMC.

KMC wako dhoofu na pengine kama watapoteza dhidi ya Azam Fc leo watajihakikishia kucheza Championship msimu ujao.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.