Ligi Kuu : TRA United, Pamba, Azam, JKT Tanzania viwanjani leo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 17th April 2026


Ligi Kuu : TRA United, Pamba, Azam, JKT Tanzania viwanjani leo

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo mzunguuko wa 19 ambapo mechi mbili zitapigwa mikoa ya Arusha na Dar es salaam.

TRA United ikiongozwa na winga aliyeteka vyombo vya habari hivi karibuni Ramadhan Chobwedo, itakuwa mwenyeji wa Pamba Jiji katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Ni vita ya kuwania nafasi ya sita, kama TRA United watashinda mchezo huo wataiondoa Pamba Jiji katika nafasi ya sita kwnai watafikisha alama 27.

Kwa sasa Pamba Jiji wako nafasi ya sita wakiwa na alama 26 wakati TRA United wako nafasi ya 7 wakiwa na alama 24.

Mchezo mwingine utapigwa saa 1 usiku Azam FC wakiwakaribisha JKT Tanzania. Licha ya kuwa matokeo ya mchezo huo hayaweza kibadili chochote kwa kila timu kwenye msimamo wa ligi, lakini ushindi kwa utawahakikishia kujiweka salama katika vita ya kuwania nafasi nne za juu.

Azam Fc wako nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 34 wakati JKT Tanzania wanashika nafasi ya nne wakiwa na alama 29.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.