Ligi Kuu; Yanga dhidi ya Mbeya City, Mashujaa uso kwa uso na Singida BS

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th April 2026


Ligi Kuu; Yanga dhidi ya Mbeya City, Mashujaa uso kwa uso na Singida BS

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi mbili zinatarajiwa kupigwa jijini Dar es salaam na mkoani Kigoma.

Vinara wa ligi hiyo Yanga watakuwa dimba la KMC Complex kuikabili Mbeya City katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Ushindi kwa Yanga utawahakikishia Wananchi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi huku Mbeya City nao wakihitaji kufanya vyema katika mchezo huo ili kujiweka katika eneo salama kuepuka kushuka daraja.

Mchezo mwingine utapigwa mapema mkoani Kigoma ambapo Mashujaa Fc watakuwa wenyeji wa Singida BS. mtanange utakaopigwa saa 10 jioni.

Mkufunzi wa Mashujaa Fc Jamhuri Kiwhelo 'Julio' atakuwa akisaka ushindi wake wa kwanza kwenye ligi tangu akabidhiwe mikoba ya kuinoa timu hiyo.

Hata hivyo anakwenda kukabliana na Singida BS ambayo ni hivi karibuni imetangaza benchi jipya la ufundi ikimuajiri Mcongomani Papy Kimoto kuwa Meneja Mkuu wa timu hiyo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.