Larry Bwalya sasa kukamilisha usajili wake Pamba Jiji

Joel JJ By Joel JJ β€’ 24th April 2026


Larry Bwalya sasa kukamilisha usajili wake Pamba Jiji

Kiungo fundi wa kimataifa wa Zambia ambaye amewahi kutamba na klabu ya Simba, Larry Bwalya, yuko hatua za mwisho kujiunga na Pamba Jiji baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano ya kisheria kuhusu usajili wake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa, mchakato wa awali wa usajili huo ulikwama kutokana na mkataba wake na klabu ya Napsa Stars ya nchini Zambia. Hata hivyo, sasa changamoto hiyo imepatiwa suluhu baada ya makubaliano kufikiwa kwa lengo la kumlinda mchezaji pamoja na maslahi ya klabu husika.

Bwalya anatarajiwa kujiunga rasmi na kikosi hicho cha mkoani Mwanza kuelekea msimu wa 2026/27, mara atakapomaliza mkataba wake wa sasa na klabu yake.

Taarifa zinaeleza kuwa Pamba Jiji tayari imeanza utekelezaji wa makubaliano hayo kwa kutoa sehemu ya ada ya usajili, huku kiasi kilichobaki kikitarajiwa kulipwa mara mchezaji huyo atakapowasili rasmi kuanza majukumu yake.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.